SERIKALI YA ZANZIBAR YAPONGEZA UZALISHAJI WA FILAMU YA VUTA N’KUVUTE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana pamoja na wamiliki wa Filamu ya VUTA N’KUVUTE kwa kuipa sifa Zanzibar katika ngazi ya kimataifa kupitia tasnia ya uwigizaji wa filamu. Rais Dk. Mwinyi alisema hayo kupitia hotuba yake